whatsapp wanawaletea feature ya ku-share screen kwenye whatsapp.
Feature hiyo inawawezesha mtumiaji wa simu kumuelekeza mwenzie juu ya kitu kilichopo kwenye simu yake.
Hii hufanyika kwa kufanya screen recording broadcast..
Mfano.
Umepata shida kwenye simu yako juu ya kitu flani na unataka kuelekezwa namna ya kukirekebisha.
Hii feature itamsaidia anaekuelekeza kupata screen record ya simu yako na kukuelekeza cha kufanya. Sasa utawezaje kufanya hivyo?
Ingia Whatsapp kisha piga video call.Chini ya video call, Unayempigia akishapokea utaona kialama cha screen sharing ambacho ni simu yenye mshale. Utabonyeza hicho!Kwa mara ya kwanza itakwambia maneno "screen sharing is private..." Hivyo utabonyeza continue
Hivyo atakuwa na uwezo wa kukupa maelekezo nini cha kufanya kwenye aimu yako ili kutatua shida yako.
Feature hii ipo kwenye telegram tangu 2017.